Jumatano 29 Oktoba 2025 - 09:53
Mahakama ya mwisho ya Palestina ilihitimishwa kwa kukumbushia miaka mingi ya mateso waliyo pitia watu waliodhulumiwa

Hawzah/ Falk, mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika mahakama ya mwisho ya Palestina huko Istanbul alisema: “Janga la watu wa Ghaza lilianza karne moja iliyopita na linaendelea.”

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Bw. Falk, mwandishi wa ripoti wa Umoja wa Mataifa, katika hotuba yake kwenye kikao cha mwisho cha mahakama ya Palestina alisema kuwa; mauaji ya halaiki bado yanaendelea. Aliendelea na hotuba yake huku akilaani vikali usitishwaji wa taarifa zinzohusiana na mgogoro mkali unao endelea huko Ghaza na kusema:

“Janga la watu wa Ghaza halikuanza tarehe 7 Oktoba bali lilianza karne moja iliyopita na linaendelea.”

Aliongeza kwa kusema: Mauaji ya halaiki yanayoendelea Palestina na dhulma vina mizizi katika karne moja ya ukoloni. Dunia ijue kuwa ikiwa Israel na washirika wake wataruhusiwa kukwepa haki, basi dunia imethibitisha mojawapo ya uhalifu mkubwa zaidi katika kihistoria na hili litawaathiri wote.

Mahakama hii haikuwaheshimu tu wakazi wa Ghaza wa leo bali pia Wapalestina kote duniani ambao kwa miaka mingi wamevumilia mateso na uhamishwaji kutokana na dhulma na uhalifu.

Falk alidai: Mpango uliopendekezwa na Trump, Rais wa Marekani, na Macron, Rais wa Ufaransa, ni mpango mbovu kwa sababu bado unatoa nafasi ya kuendelezwa mauaji ya halaiki na ubaguzi wa Israel.

Vikao vya wazi vya siku nne vilivyofanyika kuanzia Alhamisi hadi Jumapili katika Chuo Kikuu cha Istanbul vilikuwa na matokeo chanya kutokana na juhudi za mwaka mzima za wanasheria wa kimataifa, wanasayansi na wawakilishi wa jamii ya kiraia kuhusiana na uandishi wa nyaraka za kile kinachotajwa kuwa ni uhalifu wa Israel dhidi ya Wapalestina, mbele ya kamera na macho ya umma.

Chanzo: MEDDLE EAST MONITOR

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha